Jumanne 18 Novemba 2025 - 01:07
Katika Mkutano wa “Amani Duniani” uliofanyika Jakarta Imesemwa Kwamba: Hakuna amani inayodumu bila nguvu

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Taqrib baina ya Madhehebu ya Kiislamu, katika Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa “Amani Duniani” uliofanyika Jakarta, alibainisha kwamba: hakuna amani yoyote inayoweza kudumu bila nguvu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarhama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam na Muslimin Hamid Shahriari, Katibu Mkuu wa Taqrib baina ya Madhehebu ya Kiislamu, katika Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa “Amani Duniani” uliofanyika Jakarta, alibainisha kwamba: hakuna amani yoyote inayodumu bila nguvu.

Kwa ushirikiano wa Ubalozi na Atashé wa Kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Indonesia, Hujjatul-Islam na Muslimin Hamid Shahriari aliwasili Jakarta kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Kimataifa wa “Amani ya Dunia”.

Mara tu alipowasili, alipokelewa na Balozi na Atashé wa kitamaduni wa Iran. Kuhudhuria vikao vya jumla na maalumu, kutoa hotuba na kukutana na watu muhimu na wenye ushawishi katika ulimwengu wa Kiislamu pamoja na kushiriki katika Baraza la Utamaduni la Ubalozi, ni miongoni mwa ratiba zake katika mkutano huu.

Wizara ya Utamaduni ya Indonesia ilifungua Mkutano wa Tisa wa Amani ya Dunia kwa umaalumu wa mwenyeji wa tamaduni mbalimbali kwa kaulimbiu isemayo: “Ulinganifu katika Utamaduni: Kukubali Tofauti, Kusherehekea Umoja”, katika Jumba la Makumbusho ya Taifa ya Jakarta. Tukio hili lilikuwa ni ishara ya ufunguzi wa mkutano huu wa kimataifa uliodumu kuanzia Novemba 9 hadi 11, 2025 (18–20 Aban), na ulihudhuriwa na zaidi ya watu 60 kutoka nchi 24 pamoja na watu 110 wa kitaifa kutoka dini mbalimbali, wanazuoni na wanaharakati wa amani.

Fazli Zon, Waziri wa Utamaduni wa Indonesia, katika hafla hiyo alisisitiza kwamba utamaduni unapaswa kuwa lugha kuu ya amani ya dunia. Amani lazima ilelewe; haijitokezi yenyewe, bali hustawi kupitia mazungumzo, kuheshimiana na ujasiri wa kuelewana.

Fazli Zon alisisitiza mada kuu ya mkutano: “Wastani wa Kiislamu na China kwa ushirikiano wa kimataifa.” Alieleza kuwa thamani za wastani katika Uislamu kama vile: wastani, usawa na uvumilivu, zinaendana na falsafa ya Kichina ya he, ren na li inayohimiza ulinganifu, maadili mema na heshima ya kimaadili. Umoja si kuondoa tofauti; hekima imo katika uwezo wa kukuza uelewano ndani ya utofauti.

Katika hafla hiyo, watu mashuhuri wa kimataifa walihudhuria wakiwemo: Din Syamsuddin, Rais wa Jukwaa la Amani ya Dunia na Mkurugenzi wa Kituo cha Mazungumzo na Ushirikiano wa Tamaduni; Bi. Atifa Yahya Agha, Rais wa Nne wa Jamhuri ya Kosovo; Tan Sri Lee Kim Yew, mwanzilishi wa Kituo cha Mafunzo ya Utamaduni Mchanganyiko cha Cheng Ho; Abbas Shoman, mshauri wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar Misri; Nahla Shabri al-Sayyidi na mabalozi kutoka Misri na Iran.

Adis Qadir, Makamu wa Spika wa Bunge la Indonesia anayehusika na masuala ya kiuchumi na kifedha, ndiye aliyetoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huu. Wajumbe wa kitaifa na kimataifa kutoka asili mbalimbali za kisiasa, kidini na kitamaduni walihudhuria.

Adis Qadir alisisitiza umuhimu wa mkutano huu kama jukwaa la kimkakati katika kuimarisha dhamira ya dunia katika amani wakati huu wa ongezeko la migogoro ya kivita, mivutano ya kijiopolitiki na misukosuko ya kibinadamu.

Alisema: “Mazungumzo baina ya tamaduni ndo ufunguo wa kuimarisha uvumilivu, kuzuia vurugu na kuitumia tofauti kama nguvu ya pamoja.”
Mazungumzo ni njia ya kusuluhisha migogoro kwa amani na kujenga fasili ya pamoja kati ya makundi tofauti. Hatupaswi kuruhusu dini kutumiwa kama kisingizio cha vurugu.

Aliendelea kueleza kuwa mkutano huu ni zao la juhudi za pamoja kati ya Kituo cha Mazungumzo na Ushirikiano wa Tamaduni na Taasis ya Utamaduni Mchanganyiko ya Cheng Ho. Vyote viwili vina dhamira ya kuchunguza thamani za wastani wa Kiislamu na fikra za Kichina kama mchango wa Asia katika kujenga dunia ya haki na maelewano.

Tan Sri Lee Kim Yew: “Amani ni miundombinu isiyoonekana ya wanadamu”

Katika uzinduzi, Tan Sri Lee Kim Yew alisema: “Leo, katikati ya Bunge la Indonesia – Nyumba ya watu na sauti ya demokrasia – tunafungua ukurasa mpya wa matumaini. Mkutano wa Tisa wa Amani ya Dunia si tukio tu; ni zawadi ya Indonesia kwa Asia na ulimwengu.”

Alisisitiza kwamba amani si ukosefu wa vita, bali ni kuwepo kwa huruma, uelewa na haki. Katika ulimwengu ambao kila mwaka vurugu huteketeza hadi asilimia 15 ya utajiri wa dunia, sauti ya amani lazima iwe juu kuliko sauti ya vita.

Amani: Kiini cha Uhai

Yusuf Kalla, Makamu wa 10 na wa 12 wa Rais wa Indonesia, pamoja na Din Syamsuddin, walikubaliana kwamba kiini cha ustaarabu wa mwanadamu ni amani.

Yusuf Kalla alisema: “Amani si dhana tu, bali ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Tunasema as-salam alaykum kila siku – hii ni dua ya amani. Kiini cha maisha yetu ni amani.”

Shahriari: Amani Haidumu Bila Nguvu

Katika siku ya pili, Hujjatul-Islam Shahriari, akiwa mmoja wa wazungumzaji wakuu, alisema: “Amani haidumu bila nguvu; kupata amani ya haki na ya kweli kunahitaji mazungumzo ya kimaadili, kupinga dhulma, na kuunda mizani baina ya nguvu ngumu na nguvu laini.”

Alieleza kwamba taasisi za kimataifa zimekuwa butu, na madola ya kibeberu yanatafuta tu maslahi yao hata kwa kumwaga damu ya wasio na hatia.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha